RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA GAWIO LA BILIONI 1.13 KUTOKA TEMESA

News Image

Posted On: November 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 1.13 ikiwa ni gawio la Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme Profesa Mhandisi Idrissa Mshoro, kwenye hafla ya kupokea gawio toka taasisi za umma iliyofanyika Ikulu Chamwino Jumapili November 24, 2019. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Mhandisi Japhet Maselle.