RAIS SAMIA ATEUA MTENDAJI MKUU MPYA TEMESA

News Image

Posted On: May 14, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameteua Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA). Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bakari S. Machumu tarehe 03 Mei, 2026 imesema, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Bwa. Kheri Abdul Mahimbali ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA).