ITENGENEZENI TEMESA IWE CHOMBO CHA KUTUMAINIWA, RAIS SAMIA
Posted On: May 14, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amempa maagizo Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Kheri Mahimbali kuhakikisha anautengeza Wakala huo na kuufanya unakuwa chombo cha Serikali cha kutumainiwa katika utoaji wa huduma za matengenezo ya magari, huduma za vivuko na ukodoshaji mitambo.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati alipokuwa akiwaapisha viongozi aliowateua tarehe 6 Mei, 2026 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
''Kwahiyo nenda kayasimamie muende mkaitengeneze TEMESA iwe kweli ni chombo cha Serikali cha kutumainiwa, sina shaka na uwezo wako na nadhani 'you are grown up', nenda kayasimamie.'' Alisema Rais Samia.