KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AKAGUA UJENZI WA KIVUKO MV.UKARA

News Image

Posted On: October 09, 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga leo amefika katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV.UKARA kinachoendelea kujengwa.

Katibu Mkuu ameongozana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle ambapo ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa mpaka sasa ambapo mkandarasi anayesimamia ujenzi huo Major Songoro amemuhakikishia kwamba kivuko hicho kitakua kimefika Bugorola Ukara ifikapo katikati ya wiki ijayo.