KATIBU MKUU UJENZI APOKEA KIVUKO CHA MV.PANGANI II BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI
Posted On: October 21, 2020
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch.Elius Mwakalinga leo amekipokea rasmi kivuko cha MV.PANGANI II kilichofanyiwa ukarabati mkubwa katika sherehe zilizofanyika Wilayani Pangani mkoani Tanga leo. Kivuko cha MV. PANGANI II kimefanyiwa ukarabati kwa gharama ya shilingi milioni 496 na kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari madogo 4 sawa na tani 50. Kivuko hicho kinatoa huduma kati ya Pangani na Bweni Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah.