MWENYEKITI MPYA WA BODI YA USHAURI TEMESA ATAMBULISHWA, AITAKA KUWA NA MTAZAMO MPYA

News Image

Posted On: October 10, 2025

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Bw. Andrew Massawe ametambulishwa rasmi leo kwa menejimenti ya wakala huo.

Halfa hiyo fupi ya utambulisho imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wakala huo ulioko Mtaa wa TEMESA Tamburakeli mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa kwa menejimenti ya Wakala na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala, Mwenyekiti wa Bodi amesema TEMESA ina wajibu mkubwa sana kama Taasisi kuhakikisha mkakati wake wa mabadiliko unawafikia wadau wake unaowahudumia ambao ni Taasisi za Umma na Serikali.

“ Ninaamini kwa Taasisi hii tukifanya kazi kwa kushirikiana, kuwa wawazi, waadilifu na wenye ushirikiano na tukaunganisha nguvu na uzoefu basi tutasonga mbele.” Amesema Bwana Massawe.

Mwenyekiti pia ameshauri menejimenti kuwa na mtizamo mpya hasa upande wa kibiashara ambapo amewataka viongozi kubadilika na kuwaza kibiashara kwakuwa Taasisi inatakiwa kujiendesha.

Bwa. Massawe pia ameiagiza menejimenti kuhakikisha watumishi wanapewa mafunzo ya mara kwa mara pamoja na kupewa motisha ili waweze kufanya kazi kwa moyo na uadilifu.