Nane Nane 2018 Nyakabindi
Posted On: August 02, 2018

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unashiriki maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu.
Katika banda la TEMESA utapata huduma ya
1. kupimiwa gari bure kwa kutumia kifaa cha kielektroniki cha kubaini magonjwa ya magari
2. Maelezo ya namna sahihi ya kutumia taa za barabarani
3. Kujifunza matumizi salama ya vivuko na ukodishaji mitambo ya serikali inayosimamiwa na TEMES
4. Huduma za ushauri katika nyanja za uhandisi mitambo, elektroniki, na viyoyozi
