MWENYEKITI BODI YA USHAURI AZURU TEMESA
Posted On: September 24, 2019
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Profesa Eng. Iddris Bilali Mshoro amezuru katika ofisi za Wakala huo sambamba na wajumbe wa bodi hiyo ambapo pamoja na kuzungumza na viongozi waandamizi, walipata fursa ya kutembelea karakana ya Wakala huo ya MT. Depot iliyopo Keko jijini Dar es Salaam na kujionea jinsi shughuli mbalimbali za utendaji kazi zinavyoendelea katika karakana hiyo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala huo.