MKUU WA MKOA MWANZA AKAGUA UJENZI KIVUKO KIPYA CHA BUGOROLA UKARA
Posted On: October 06, 2020
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha Bugorola Ukara (MV. UKARA II) ambacho ujenzi wake unaendelea katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza. Kivuko hicho kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa wiki hii kabla ya kushushwa kwenye maji ili kufanyiwa majaribio ya mwisho na kupelekwa Ukara Bugorola kwa ajili ya kuanza kutoa huduma mara baada ya taratibu zote za kukipima uwezo wake na usalama kukamilishwa na mamlaka zinazohusika ikiwemo TASAC.