KIVUKO CHA MV UKARA II NJIANI KUELEKEA BUGOROLA UKARA

News Image

Posted On: October 18, 2020

Kivuko kipya cha MV.UKARA II HAPA KAZI TU kimeanza safari ya kuelekea visiwa vya Ukerewe katika maeneo ya Bugorola Ukara kwa ajili ya kuanza kutoa huduma. Kivuko hicho kimeanza safari mapema asubuhi ya leo ambapo kinategemewa kuzinduliwa hapo kesho na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe katika sherehe zinazotarajiwa kufanyika katika kisiwa cha Ukara.

Wananchi wa Bugorola, Ukara pamoja na maeneo ya karibu wanakaribishwa hapo kesho kufika kujionea tukio hilo la kihistoria la uzinduzi wa kivuko hiko kipya.