KIVUKO MV. KYANYABASA CHASIMAMA KUTOA HUDUMA BAADA YA SERIKALI KUANZA UJENZI WA DARAJA MTO NGONO

News Image

Posted On: July 25, 2025

Mhandisi Lukombe King'ombe Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) akikagua kivuko cha MV. KYANYABASA ambacho kilikuwa kinatoa huduma katika Mto Ngono kati ya eneo la Kata ya Kasharu iliyoko Wilaya ya Bukoba Vijijini na kata ya Buganguzi iliyoko Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.

Kivuko MV. KYANYABASA kimeacha kutoa huduma eneo hilo baada ya Serikali kuanza ujenzi wa daraja jipya litakalounganisha kata hizo mbili na vijiji vya jirani.

Kivuko cha MV. KYANYABASA kilinunuliwa mwaka 2005 na kinao uwezo wa kubeba abiria 50 na magari madogo mawili kwa pamoja.

Ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kurahishisha kwa kiasi kikubwa usafiri kwa wakazi wa kata hizo na kata za jirani.