MV.KAZI SASA KUREJEA NOVEMBA MWISHONI
Posted On: November 12, 2022
“Leo hii tumekuja hapa kwenye yadi hii ya mkandarasi Songoro kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV KAZI. Kazi inakwenda vizuri na vitu vyote ambavyo vinapaswa kuwa vimeshafika, injini zote kama mnavyoona, gia boksi, jenereta, kila kitu kipo hapa na mkandarasi ametuahidi kwamba anafanya kazi usiku na mchana matarajio ni kua anakamilisha ufungaji wa vifaa hivi ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Novemba.” Lazaro N. Kilahala. Mtendaji Mkuu TEMESA akikagua ukarabati wa kivuko hicho unaoendelea katika Yadi ya Songoro iliyopo Kigamboni jijiniDar es Salaam Tarehe 11 Novemba 2022.