MTENDAJI MKUU TEMESA MHANDISI JAPHET Y. MASELLE AFANYA ZIARA MKOA WA PWANI

News Image

Posted On: March 13, 2019

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle amefanya ziara ya kikazikatika mkoa wa Pwani ambapo amekutana na wafanyakazi wa TEMESA mkoani humo.

Akiwa mkoani humo, Mhandisi Maselle alitembelea karakana ya wakala huo wilayani Kibaha na kujionea shughuli za utendaji kazi zinavyoendelea ambapo alipata fursa ya kukagua baadhi ya mitambo iliyopo katika karakana hiyo, akiba ya vipuri kwa ajlili ya huduma kinga ya magari, pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa mkoa huo na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kituo hicho.

Miongoni mwa changamoto zilizoibuliwa na wafanyakazi hao katika kikao hicho ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi ikiwemo spana, jeki, baadhi ya huduma kama mashine ya kupima uwiano wa gari na matairi pamoja na upungufu wa wafanyakazi hasa katika kitengo cha umeme na makenika ambapo Kaimu Mtendaji mkuu aliahidi kuwapelekea mafundi katika kada hio mara tu nafasi zao zitakapotolewa hivi karibuni na tume ya ajira. ‘’Tumepata nafasi ishirini na sita za kuajiri na katika hizo kuna mafundi wataajiriwa kwa hiyo kuweni tayari wakati wowote zitatangazwa na tume na wakishamaliza usaili nitawaletea watumishi hapa kujaza hizo nafasi’’, alisema Mhandisi Maselle.

Naye Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Richard Mutagulwa amewasisitizia wafanyakazi hao pamoja na watendaji wake kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea ambapo kwa mwaka huu wa fedha mkoa huo unategemewa kuzalisha jumla ya shilingi milioni ……

Aidha, akiwa katika kikao hicho aliwataka wafanyakazi wa mkoa huo kujipanga kikamilifu kuhakikisha huduma zinaboreshwa na kuzipatia utatuzi lawama ambazo mara nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa karakana za wakala huo na baadhi ya wadau, aliwataka kutoa ushirikiano mzuri kwa wadau wanaotumia huduma za wakala na kuwasisitizia kutoa huduma iliyo bora ili kuendelea kuwashawishi kupeleka kazi zao TEMESA.