MTENDAJI MKUU TEMESA AKABIDHI MTAMBO KWA CHUO CHA UJENZI MOROGORO
Posted On: February 18, 2020
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amekabidhi mtambo kwa Chuo cha Ujenzi Morogoro (MWTI), mtambo huo ambao ni Greda la kuchongea bararaba ulikuwa ukitumiwa na karakana ya TEMESA Mkoa wa Morogoro, hafla ya kukabidhi mtambo huo imefanyika chuoni hapo ambapo imehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo hiko Mhandisi Melkizedeck L. Mlyapatali pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mtambo huo utatumika kufundishia wanafunzi kwa vitendo pamoja na kuingizia kipato chuo hiko kwa kufanya shughuli za ukodishaji. Pamoja na mtambo huo chuo hiko pia kimekabidhiwa kompyuta ambazo zimetolewa na katibu Mkuu kwa ajili ya shughuli za kimasomo chuoni hapo.