MTENDAJI MKUU TEMESA AFUNGA MAFUNZO IPSAS

Posted On: May 14, 2018
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu mwishoni mwa wiki hii amewatunuku vyeti wahasibu wa wakala huowaliohitimu mafunzo yaUfungaji wa Hesabu za Serikali kwa mfumo wa IPSAS.
Mafunzo hayo yalichochukua muda wa siku tano yaliendeshwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Ernst and Young katika ukumbi wa mikutano uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wahasibu hao mara baada ya kuwatunuku vyeti Dkt. Mgwatu aliwapongeza kwa kumaliza mafunzo hayo na kuwataka kutumia ujuzi walioupata kuleta maendeleo katika wakala huo. “Mafunzo mliyoyapata yawe chachu ya ufanisi wenu katika kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu, umakini na weledi wa hali ya juu ili kuuletea wakala wetu tija kwa taifa”. Alisema Dkt Mgwatu.
Serikali kwa sasa inatekeleza mpango mkakati wa kuhakikisha taasisi zake zinandaa mapato yake kwa kutumia viwango vya kimataifa vya Uhasibu katika sekta ya Umma yaani IPSAS. Mfumo huo hutumika kukusanya hesabu za mapato na matumizi ya serikali na kuiwezesha kutambua kikamilifu hesabu za mali, madeni na makusanyo ya kodi. Matokeo ya utekelezaji wa mfumo huo yanaiwezesha serikali kutoa taarifa za uwazi katika taasisi zake na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango.