MKUU WA WILAYA MOROGORO AIPONGEZA TEMESA KWA MIKAKATI YA UBORESHAJI HUDUMA

News Image

Posted On: March 27, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeka Nhemwa ameipongeza TEMESA kwa jitihada zake za uboreshaji wa huduma kwa kutumia vifaa vya kisasa na kuahidi kuwa balozi atakaeitangaza vyema Taasisi hiyo.

Akizungumza katika kikao cha wadau kilichofanyika Mkoani Morogoro tarehe 22 Machi katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, Mhe. Nhemwa amesema ameona vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya utendaji kazi ambapo pia amepata fursa ya kushuhudia namna ya kugundua matatizo ya gari kwa kutumia vifaa ya kisasa zaidi (Diagnosis Machine)

Nhemwa amewapongeza TEMESA kwa kuweza kuainisha matatizo yao ya ndani naya nje na kuyapatia ufumbuzi kwa kupita Mikoa yote Tanzania na kutoa elimu kwa wadau wanaonufaika na huduma wanazotoa.

“Niwasifu TEMESA imeweza kuainisha matatizo yao ya ndani na nje wakaja na ufumbuzi wakaona sasa wapite kwa wadau wanaowahudumia Tanzania nzima ili waweze kuwaeleza changamoto zao na mikakati ya kurekebisha tatizo hili”, alisisitiza.

Aidha Mhe. Nhemwa ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweza kuisimamia vyema TEMESA kwa kuwawezesha kuelezea utatuzi wa changamoto zilizokuwa zinawakabili.

Naye Mkurugenzi wa Huduma Saidizi TEMESA Bi.Josephine Matiro amesema katika utekelezaji wa majukumu ya TEMESA tangu kuanzishwa kwake, wametambua na kujitathmini na wamekutana na changamoto mbalimbali za kiutendaji na kuamua kufanya marekebisho.