MAAFISA USAFIRISHAJI ZADI YA AROBAINI KUTOKA TANESCO WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA KIDIGITALI WA MUM
Posted On: June 23, 2025
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania(TEMESA) umetoa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo wa Kidigitali wa usimamizi wa kazi za matengenezo maarufu kama MUM kwa maafisa usafirishaji zaidi ya 40 kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Akizungumza mara baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Mkoani Mwanza, Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Frank Jackson amesema kuwa wametoa mafunzo hayo ili kuendelea kurahisaha utoaji huduma kwa wadau wao.
Akifunga mafunzo hayo Margaret Peter ambaye ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala (TANESCO) amesema kuwa kongamano hilo la maafisa usafirishaji ni muhimu kuwa endelevu ili kuendelea kuwajengea uwezo maafisa hao.
Mfumo huo wa MUM unapatikana kupitia tovuti ya mum.temesa.go.tz