MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI YAFANYIKA KITAIFA MKOANI NJOMBE
Posted On: May 14, 2026
Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania- TEMESA, leo tarehe 1 Mei, 2026 wameungana na Wafanyakazi wengine Mkoani Njombe kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani “Mei Mosi. ” Maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji Mkoani Njombe.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, amewaasa wafanyakazi kuwa na utendaji kazi wenye stara na utu kuendana na kauli mbiu ya Kazi na Utu, Tunasonga Mbele” ili kufikia dira ya maendeleo ya Taifa na kuhakikisha ifikapo mwaka 2050 Taifa linafikia ukuaji wa kasi kiuchumi.
“Maadhimisho ya mwaka huu yanaonesha uelewa wa watumishi wetu katika kuifikia dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 kwa kutangaza Heshima, Utu na Usawa kwa wafanyakazi. Wafanyakazi ambao ni nguzo na msingi mkubwa wa taifa letu inatupasa kuzingatia lengo namba 8 la maendeleo endelevu katika utumishi linalohusu kazi zenye staha na utu unaojengwa na nguzo kuu nne, ambazo ni upatikanaji wa ajira, Ulinzi wa haki kazini, Hifadhi za jamii na ushirikishwaji mahala pa kazi kazi. Haya yote yatakuwa na maana kama yatagusa maisha na ustawi wa wafanyakazi. Utekelezaji wa dira ya ukuwaji kiuchumi unawategemea sana ninyi wafanyakazi kutoa mchango mkubwa katika kuyafikia. Hivyo Serikali itaendelea kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa watumishi kwa kuendelea kuboresha mazingira yenye staha kwa kundi hili kwa Sekta za Umma na Binafsi. Amesema Mhe. Rais. Dkt. Samia.
Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani “Mei Mosi mwaka 2026 yamebebwa na Kauli mbiu inayosema “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika utekelezaji wa Dira 2050.”