MEI MOSI 2021
Posted On: May 01, 2021
Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) leo wameshiriki maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi. Maandamano hayo yameanzia viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo yamehusisha wafanyakazi wote wa Sekta binafsi pamoja na Serikali yakiwa na Kauli Mbiu “Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee”. Kitaifa Sherehe za Mei Mosi zinafanyika Mkoani Mwanza ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.