Masauni atembelea banda la TEMESA (SABASABA)

News Image

Posted On: July 13, 2018

Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewataka TEMESA kuhakikisha wanalipatia suluhisho suala la vipuri feki vinavyofungwa kwenye baadhi ya magari hapa nchini. Mhandisi Masauni ameyasema hayo mapema leo wakati alipotembelea banda la TEMESA katika Maonesho ya kimataifa ya 42 ya Biashara maarufa kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.