MAADHIMISHO YA WIKI YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KITAIFA DODOMA YAMALIZIKA

News Image

Posted On: September 02, 2018

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Thobias Andengenye, mwishoni mwa wiki hii amefunga rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji yaliyokua yakifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwa kuwapa vyeti vya ushiriki wadau wa mashirika mbalimbali walioshiriki maadhimisho hayo na pia kuwataka kuyapa vipaumbele masuala ya usalama makazini kwa kufunga ving'amua moto ili kuepusha majanga ya moto yanayoweza kutokea bila taarifa. Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki maadhimisho hayo pia ambapo ilipatiwa cheti cha ushiriki kilichopokelewa na mwakilishi kutoka kikosi cha umeme Bi. Godliver Rweyemamu.