UKOSEFU WA VIVUKO VYA SERIKALI MAGOGONI, CHANGAMOTO KUBWA WANANCHI DAR ES SALAAM
Posted On: May 12, 2025
Kukosekana kwa vivuko vya serikali kwa ajili ya kuwavusha wananchi wa maeneo ya wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam imeendelea kuwa changamoto isiyokuwa na muarobaini wa kudumu wa mamlaka hiyo.
Pamoja na juhudi za serikali kuleta mwekezaji mpya kutoka kampuni ya Azam Marine kwa ajili ya kusaidia katika usafirishaji wa kuvusha watu na mizigo katika eneo la Magogoni Feri Dar es Salaam, uhakika wa kuvuka kwa abiria bado ni changamoto.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Rada umebaini kuwa, tangu mwezi juni mwaka 2024, huduma za kuvusha abiria katika eneo hilo ni kivuko kimoja tu cha serikali MV Kazi ambacho ndiyo kinachotumika kuvudha abiria huku vivuko vingine viwili vikiwa kwenye matengenezo makubwa
Matengenezo ya vivuko hivyo yanafanyika katika karakana za makampuni ya nchi mbili ambazo ni Kenya, Mombasa na Kampuni ya Kitanzania Songoro Marine ya jijini Dar es Salaam.Vivuko hivyo ni MV Kigamboni ambayo inatengenezwa na Songoro Marine wakati MV Magogoni inatengenezwa nchini Kenya -Mombasa.
Changamoto kubwa ambayo inatajwa na wananchi katika kukosekana kwa vivuko vya serikali ni apmoja na adha ya wanayoipata abiria wakati wanavuka kuelekea sehemu zao za kazi wakati wa asubuhi au wanaporudi majumbani mwao nyakati za jioni.
Pia suala la nauli ni kikwazo kwani vivuko vya Serikali nauli zake ni shilingi 200/= wakati nauli ya mwekezaji Azam Marine ni shilingi 500/=, ambayo baadhi ya wananchi wanalalamika kwamba inakuwa changamoto kwao wanapokuta kivuko cha serikali kimeharibika na kutakiwa kutumia usafiri wa mwekezaji.
“Hali inakuwa mbaya sana tunapokuta kivuko cha serikali kimepata hitilafu kwa sababu wakati mwingine unakuta mtu anashilingi 400/= tu ya kwenda na kurudi. Lakiniunapokuta vivuko vya Azam Marine unatakiea uwe na shilingi 1000 kwenda na Kurudi kwa ajili ya kuvuka tu maji” anasema Hawa Hamisi mwananchi wa Mwembe Mtengu Tuangoma Temeke.
Anasema yeye ni mfanyabiashara wa samaki za kukaanga hivyo kutumid shilingi 1000/= pekee kwa ajili ya kuvukq maji ni hasara kubwa kwa sababu kabla ya kuvuka maji anatakiwa alipe shilingi 2000/= kwenda na kurudi kutoka Kigamboni hadi Tuangoma.
Anasema yeye ni mfanyabiashara wa samaki za kukaanga, hivyo kutumia shilingi 1000/= pekee kwa ajili ya kuvuka maji ni hasara kubwa, kwa sababu kabla ya kuvuka maji anatakiwa kulipa shilingi 2000/= kwenda na kurudi kutoka Kigamboni hadi Tuangoma.
“Ukilipa shilingi 1000/= ya Azam Marine na shilingi 2000/= za daladala, basi nitatakiwa kulipa jumla ya shilingi 3000/= za nauli ambazo ni changamoto kutokana na mitaji yetu midogo ya samaki,” anasema.
Wengine wanaoathirika na changamoto ya nauli ni wanafunzi wa vyuo wanaoishi katika maeneo ya Kigamboni na sehemu za jirani kama Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Utumishi Magogoni, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (hiki kipo upande wa Kigamboni).
“Wengine tuna kadi kabisa ambapo tayari wazazi wametuwekea nauli ya mwezi mzima ya shilingi 200/= kwa ajili ya kutumia vivuko vya serikali, hivyo mabadiliko ya mfumo wa gharama kwa kutumia vivuko vya mwekezaji ni usumbufu mkubwa. Hii changamoto inawakumba sana sasa na unombe mwanzoni akaongezewe nauli ili kuvuka ng’ambo” alisema Jonas Haule mwanafunzi wa mwaka wa pili kutoka IFM.
Wengine wanaoathirika na kukosekana kwa vivuko vya serikali ni abiria ambao wanavuka na magari yao na mizigo mbalimbali ambapo vivuko vya Azam Marine vinaruhusu hivyo wakilazimika kuvunjika mjini na kutumia daraja la Nyerere NSSF.
Akiongea na gazeti hili ofisini kwake Meneja wa vivuko Kanda ya Mashariki Abrahaman Amir amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa vivuko vya serikali lakini alisisitiza “wanapambana nazo”.
Alisema katika eneo la Magogoni Feri, wanachangamoto tangu vivuko viwili viondolewe kwa ajili ya matengenezo makubwa kwa mujibu wa utaratibu mwezi Juni 2024.
“Tangu June mwaka jana, tukiwa na kivuko kimoja tu cha MV Kazi ndicho kilichokuwa kikihudumia watu kwa kushirikiana na vivuko vingine vya mwekezaji vya Azam Marine. Tunapopata changamoto mwekezaji anatusaidia kuvusha watu” alisema.
Alisema wakati kivuko cha serikali kinapopata changamoto ya hitilafu au kupumzishwa kwa ajili ya matengenezo madogo ambayo ni lazima, wanakuwa wameweka taarifa na kwa wale ambao tayari wanaouziwa tiketi wote husafirishwa na kivuko vya mwekezaji kwa nauli hiyo hiyo ya shilingi 200/=, na wanafunzi waliovaa sare za shule huvuka bure.
“Mwananchi yeyote anayeonekana tayari amekata tiketi anasafirishwa na mwekezaji kwa nauli ya serikali, na wengine wanaouzwa bado hawajakuta tiketi wanapewa taarifa kwa ajili ya kutafuta usafiri mbadala. Mara nyingi kivuko chetu hakichelewi kwenye matengenezo, kinawasa kuchukua angalau kama saa moja hivi halafu kinarudi kufanya kazi,” alisema.
Meneja huyo alibainisha kuwa vivuko vyote vilivyopelekwa kwenye matengenezo haya ya matengenezo yanaendelea vizuri akitolea mfano wa MV Magogoni matengenezo yake yamefikia asilimia 80 na miezi michache ijayo kivuko hicho kitarudi kufanya kazi.
“Vivuko vyetu matatengenezo yanaendelea vizuri. MV Magogoni kilichopo Songoro Marine kimefikia asilimia 80 na MV Kigamboni kilichopo Mombasa ni asilimia 10, tunashukuru serikali kwa kuchukua dhamana ya matengenezo,” alisema.
Naye Mkuu wa Kituo cha huduma za vivuko cha Magogoni Feri, Hassan Madohora alisema wanajitahidi kupambana na dharura zote ili kuhakikisha wananchi wanavuka bila usumbufu wowote.
Alisema wanachukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kuwajulisha wananchi wakati vivuko vyao vinapopelekwa kufanyiwa matengenezo.
“Changamoto ipo lakini lazima vivuko vifanyiwe maintenance (matengenezo). Kwa mfano kivuko chetu kinapumzika kwa ajili ya matengenezo kwa masaa 3 tu, hiyo kinarejea saa 21. Matengenezo ni lazima yafanyike hata kwaenye vyombo vingine vya usafiri ikiwemo tunapopata dharura ya matengenezo tunawajulisha wananchi wetu,” alisema.
Kituo cha huduma cha Magogoni Feri kina vivuko vitatu vya serikali ambavyo ni MV Kigamboni, MV Kazi na MV Magogoni huku mwekezaji kampuni ya Azam Marine ikidairiwa kuwa na vivuko sita.
Vivuko vya Azam Marine (sea taxis) kila kimoja kina uwezo wa kubeba abiria 250 hadi abiria bado ni ndogo ukilinganisha na wengi wanaovuka eneo hilo kila siku.