KIVUKO CHA BILIONI 5.3 KUTUA MAFIA NYAMISATI FEBRUARI MWAKANI

News Image

Posted On: October 28, 2019

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Elias Kwandikwa amezindua ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 sawa na tani 100, kinajengwa kwa shilingi bilioni 5.3 za Kitanzania na kitakamilika ifikapo mwezi Februari mwakani.