KIKAO KAZI CHA MENEJIMENTI ZA UJENZI

News Image

Posted On: June 10, 2023

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA ),Lazaro Kilahala pamoja na Menejimenti ya Wakala huo leo wamehudhuria Kikao Kazi kati ya Menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Menejimenti za Taasisi za Sekta hiyo kilichofanyika mjini Tanga. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Tanga Beach Resort n na kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour kikiwa na lengo la kuimarisha Ari na Morali katika utendaji kazi.