KATIBU MKUU UJENZI ATEMBELEA TEMESA
Posted On: March 13, 2019
KATIBU MKUU UJENZI ATEMBELEA TEMESA:
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga ametembelea Makao Makuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kujionea Majukumu yanayotekelezwa na Wakala huo.
Akiwa ofisini hapo, Katibu Mkuu alipewa maelezo Kuhusu Majukumu Mbalimbali ya Wakala, mafanikio na changamoto za utekelezaji wa majukumu hayo. Pia aliweza kutembelea karakana ya Mt. Depot ambapo alikagua vifaa vipya vya karakana ambavyo vimenunuliwa kwa ajili ya kusambazwa katika mikoa mbalimbali ili kuongeza uzalishaji.
Awali, Katibu Mkuu alipata fursa ya kuongea na manejimenti ya Wakala huo ikiongozwa na Mtendaji Mkuu Mhandisi Japhet Y. Maselle.