WAZIRI KAIRUKI NA WAZIRI HASUNGA WATEMBELEA TEMESA NANENANE SIMIYU

News Image

Posted On: August 03, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga leo wametembelea banda la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA katika Maonesho ya Wakulima Nanenane mbayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Wakiwa katika banda la TEMESA, Mawaziri hao walipata fursa ya kujionea na kusikia kuhusu huduma mbali mbali zinazotolewa na Wakala huu katika nyanja za Ufundi, Umeme, Mitambo, Elektroniki pamoja na huduma za vivuko ambazo TEMESA inatoa katika mito na bahari nchi nzima.

#Nanenane2020 “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Chagua Viongozi Bora 2020”