SAFARI YA KUIMARISHA HUDUMA YA USAFIRI WA VIVUKO YAZIDI KUNOGA

News Image

Posted On: July 25, 2025

“Lengo la Serikali ni kuwaondoa wanachi wake kwenye usafiri wa mitumbwi na kuwapa uhakika wa usafiri.”

Mhandisi Lukombe King’ombe kushoto, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko TEMESA akizungumza mara baada ya kukagua kivuko MV. OLD RUVUVU pamoja na miundombinu yake ikiwemo majengo ambapo amesema ukarabati wa kivuko hicho tayari umekamilika na miundombini imekamilika na mpaka kufikia mwezi Septemba kivuko hicho kitaanza kutoa huduma kati ya Mayenzi na Kanyinya Wilayani Ngara Mkoani Kagera.