SIKU YA KIMATAIFA YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI
Posted On: May 03, 2023
Wafanyakazi wa TEMESA kote nchini wameungana na wafanyakazi wengine kote Duniani kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi Duniani ambapo kwa Tanzania sherehe hizo Kitaifa zimefanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro zikihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi.