​KAMATI YA MIUNDOMBINU YAPITISHA RANDAMA YA BAJETI WIZARA YA UJENZI 2026/2027.

News Image

Posted On: March 25, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imepitisha Randama ya Mpango na Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ya Wizara ya Ujenzi hatua inayotajwa kuwa muhimu katika kuendeleza kasi ya uboreshaji wa miundombinu nchini.

Akizungumza jijini Dodoma Machi 24, 2026, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso, alisema uamuzi huo unaenda sambamba na dhamira ya kuhakikisha miundombinu ya kisasa inaendelea kujengwa na kuboreshwa ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameishukuru Kamati hiyo kwa kuidhinisha randama hiyo na kuahidi kuwa Wizara itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango bora na kuleta manufaa kwa wananchi.