MUONGOZO WA MATUMIZI YA “WALLET”

News Image

Posted On: September 29, 2025

  • 1.WATEJA KUWEKA FEDHA KWENYE WALLET
  • 1.1.Usajili wa Taasisi

1.1.1.Ili kutumia “Wallet”, taasisi inapaswa kusajiliwa kwenye mfumo wa MUM.

1.1.2.Usajili utahusisha majina ya maafisa wasiopungua watatu:

  • i.Mtumishi kutoka idara tumizi,
  • ii.Mtumishi kutoka idara ya uhasibu, na
  • iii.Mkuu wa Taasisi.
  • 1.2.Kufungua Akaunti ya Wallet

1.2.1.Baada ya usajili kukamilika, taasisi itafungua akaunti ya “Wallet” kupitia Sub Menu ya Wallet na kufuata maelekezo yaliyopo.

  • 1.3.Kuweka Fedha

1.3.1.Taasisi inapaswa kufungua Sub Menu ya My Wallet ili kuomba kuweka fedha.

1.3.2.Baada ya taratibu zote za approvals kukamilika, taasisi itapokea Control Number ya malipo yenye kiasi kilichoombwa.

1.3.3.Baada ya kufanya malipo kupitia benki au mitandao ya malipo, salio la Wallet litasasishwa moja kwa moja kwenye mfumo wa MUM.

2.JINSI TAASISI ZITAKAVYOFANYA MATUMIZI YA WALLET

2.1.Malipo kwa Huduma za TEMESA

  1. Fedha zilizopo kwenye Wallet zitatumika kulipia huduma zote za TEMESA zinazopatikana kupitia mfumo wa MUM na pia katika vituo vyote vya uzalishaji vya Wakala.

2.2.Uchaguzi wa Njia ya Malipo

  1. Pindi taasisi itakaporidhia gharama zilizowasilishwa kupitia MUM, itachagua njia ya malipo kati ya:
    • “Wallet”
    • Kupatiwa Control Number ya huduma iliyoombwa.

2.3.Muamala Kupitia Wallet

  1. Iwapo taasisi itachagua Wallet, gharama husika zitapunguzwa kwenye salio la Wallet na kuelekezwa kwenye akaunti ya kituo kilichotoa makadirio ya kazi husika.
  2. Baada ya muamala kukamilika, mteja atapokea taarifa zifuatazo:
  • i.Kituo cha TEMESA kitakachotoa huduma,
  • ii.Namba ya matengenezo,
  • iii.Namba ya muamala wa Wallet (Wallet Transaction Number),
  • iv.Tarehe ya muamala,
  • v.Aina ya huduma, na
  • vi.Kiasi kilichotumika.

3.KUPATA TAARIFA ZA MATUMIZI YA WALLET

3.1.Upatikanaji wa Historia ya Matumizi

  • i.Mteja au taasisi inaweza kupata taarifa za matumizi ya Wallet moja kwa moja kupitia mfumo wa MUM kwenye Sub Menu ya My Wallet History.

3.2.Aina za Taarifa Zinazopatikana

  1. Kiasi kilichowekwa,
  2. Kiasi kilichotumika,
  3. Kazi zilizofanyika,
  4. Kituo kilichotoa huduma,
  5. Tarehe ya miamala,
  6. Salio lililopo, na
  7. Historia ya miamala yote iliyofanyika.