MKEMIA MKUU WA SERIKALI DKT. FIDELICE MAFUMIKO AIPONGEZA TEMESA KWA MABADILIKO YA KIMKAKATI SABASABA
Posted On: July 07, 2026
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, tarehe 06 Julai 2026 ametembelea banda la Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Dkt. Mafumiko ameipongeza TEMESA kwa mabadiliko yanayoendelea kufanyika, akisema yanaonesha dhamira ya dhati ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Natamani mtambue nyinyi ni taasisi ya kimkakati katika matengenezo ya magari na umeme, naipongeza TEMESA kwa hatua kubwa za mabadiliko mnazozifanya. Haya ni maendeleo yanayoleta matumaini makubwa kwa wananchi na yanaonesha wazi kuwa taasisi hii inaelekea kwenye ufanisi zaidi, ubunifu zaidi na huduma bora zaidi,” amesema Dkt. Mafumiko. Aidha, ameongeza kuwa jitihada hizo zinapaswa kuendelea ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kisasa, salama na zenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
TEMESA inaendelea kuwakaribisha wananchi na wadau wote kutembelea banda lake ili kupata elimu kuhusu huduma zake, ubunifu wa kiteknolojia na mchango wake katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wadau