UJENZI VIVUKO VIPYA VITANO MWANZA WAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 80%

News Image

Posted On: March 05, 2024

Ujenzi wa vivuko vipya vitano unaofanywa na Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), sasa umefikia wastani wa zaidi ya Asilimia 80%. Vivuko hivyo vipya vitano, vitakapokamilika vitakwenda kutoa huduma kati ya maeneo ya Ijinga na Kahangala Wilayani Magu, Bwiro na Bukondo Wilayani Ukerewe, Nyakaliro na Kome Wilayani Sengerema, Buyagu na Mbalika Wilayani Sengerema pamoja na Kisorya Wilayani Bunda Mkoani Mara na Rugezi Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza. Vivuko hivyo vipya vinaendelea kujengwa na Mkandarasi Songoro Marine katika Yadi yake iliyoko Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza na vinatarajiwa kuanza kukamilika kwa awamu kuanzia mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu wa 2024.