MTENDAJI MKUU TEMESA ATEMBELEA BANDA LA WAKALA NANENANE
Posted On: August 08, 2020
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle leo ametembelea banda la Wakala huo katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu ambapo Maonesho hayo yanafanyika Kitaifa. Akiwa katika banda hilo Mtendaji Mkuu alipata wasaa wa kuzungumza na waandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo aliweza pia kuwapitisha na kuwaonesha kazi mbalimbali na huduma ambazo TEMESA inatoa katika Maonesho hayo ambayo kilele chake kinafikia leo na yanatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa.