MTENDAJI MKUU TEMESA KILAHALA AKISAFIRI KWA BOTI KUKAGUA MAENDELEO YA MAEGESHO BWIRO BUKONDO

News Image

Posted On: July 25, 2025

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala akisafiri kwa boti kutokea eneo la Bukondo kwenda Bwiro Halmashauri ya Wilaya ya Nansio-Ukerewe Mkoani Mwanza kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya vivuko ambapo Kilahala amesema Serikali kupitia TEMESA tayari imekamilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko kwa pande zote mbili za Bukondo na Bwiro ambayo yatatumika na kivuko kipya MV. BUKONDO kinachoendelea na ujenzi.

Kilahala amesema kivuko hicho tayari kimefikia zaidi ya asilimia 94% ya ujenzi wake na amewaahidi wananchi wa maeneo hayo kwamba watakuwa na usafiri wa uhakika zaidi ambao utawawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo ili kuendeleza uchumi wao na kuboresha hali zao za kimaisha.