MTENDAJI MKUU TEMESA AIPONGEZA KAMATI YA UKAGUZI WA MAHESABU

News Image

Posted On: September 24, 2020

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle leo ameshiriki katika hafla fupi ya kuiaga kamati ya ukaguzi wa mahesabu yaTEMESA ilyopita na kuikaribisha kamati mpya, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa karakana ya mkoa wa Dodoma ilihusisha wajumbe wote waliokuwepo katika kamati ambayo iliundwa mwaka 2017 pamoja na wajumbe wapya ambao kamati yao iliteuliwa mwezi Aprili mwaka huu..

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhandisi Maselle aliipongeza kamati iliyopita kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kipindi kilichopita ambapo walisababisha TEMESA kupata hati safi na kuitaka kamati mpya kuiga mfano kwa kamati hiyo iliyopita kwa kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa ili kuendelea kuifanya TEMESA kuendelea kupata hati safi.

Katika hafla hiyo, Mtendaji Mkuu pia alipata wasaa wa kuwatunuku vyeti wajumbe wa kamati iliyopita pamoja na kukabidhi vitendea kazi kwa kamati mpya ya wajumbe walioteuliwa.

Mara baada ya hafla hiyo, wajumbe hao wapya walioteuliwa walipata wasaa wa kufanya kikao chao ambapo walianza kwa kuthibitisha kuhtasari wa kikao kilichopita ambacho kilifanyika mwezi Julai 2020.

Pamoja na hayo, wajumbe hao pia waliweza kupitia rasimu ya hesabu za Wakala kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020, kujadili taarifa ya robo ya nne ya mkaguzi wa ndani kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020, kujadili taarifa ya mwaka ya mkaguzi wa ndani kwa mwaa wa fedha wa 2019/2020, kujadili taarifa ya mkaguzi wa nje (CAG's recomendations 2018/2019) pamoja na kujadili taarifa ya miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.