KIKAO CHA MTENDAJI MKUU PAMOJA NA WATUMISHI WA TEMESA MAKAO MAKUU

News Image

Posted On: July 06, 2023

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Ndugu Lazaro Kilahala leo tarehe 06 Julai 2023 amefanya kikao cha ndani na watumishi wa TEMESA Makao Makuu ikiwa ni muendelezo wa vikao vya ndani vya kupeana mrejesho ili kuweza kuboresha utendaji kazi wa Wakala.

Mtendaji Mkuu aliwataka watumishi kufanya kazi kwa tija na malengo ili kuboresha Wakala kwa ujumla.

Aidha, Mtendaji Mkuu aliwaeleza watumishi kuwa Wakala unaendelea na maboresho ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA kwa nia ya kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi, baadhi ya mifumo ambayo wakala unaendelea kuboresha na kutumia ni E-office, Stock management, Pos Management, Fuel Management system na Motor vehicle management information system.