MTENDAJI MKUU AKABIDHI GARI MBILI MPYA DODOMA NA PWANI

News Image

Posted On: November 25, 2021

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle leo amekabidhi gari mbili mpya zilizonunuliwa na Wakala huo kwa ajili ya kuboresha huduma za karakana nchini.

Gari hizo mpya aina ya Toyota Hilux, zimekabidhiwa kwa mameneja wa Mikoa ya Dodoma na Pwani ambao wameushukuru Wakala kwa kuwapatia magari hayo na kuahidi kuyatumia vizuri kwa ajili ya kuwaongezea makusanyo na kuyatunza ili yadumu kwa muda mrefu.

Magari hayo mawili ni kati ya magari 14 ambayo yamenunuliwa na Wakala huo na yanatarajiwa kusambazwa katika mikoa mbalimbali nchini.