MAKADIRIO YA BAJETI 2024/2025

News Image

Posted On: May 29, 2024

Serikali ya Awamu ya sita imepata mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za vivuko kupitia TEMESA Katika kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Mei 2024.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akiwasilisha mpango wa makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2024/25 Bungeni jijini Dodoma.

Amesema Wizara imeendelea na ujenzi wa vivuko vipya 8 ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kusisitiza kuwa vivuko hivyo vitakapokamilika vitatumika kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

Alivitaja vivuko hivyo kuwa ni Bwiro – Bukondo(Ukerewe), Kisorya (Bunda) – Rugezi (Ukerewe), Ijinga – Kahangala (Magu), Nyakaliro – Kome (Sengerema), Buyagu (Sengerema) – Mbalika (Misungwi), Mafia – Nyamisati (Rufiji) na Magogoni (Ilala) – Kigamboni (Kigamboni).

Aidha Bashungwa amesema kuwa Serikali itahakikisha mkandarasi M/S Songoro Marine analipwa fedha zote ili akamilishe ujenzi wa vivuko hivo ndani ya mwaka huu wa fedha.