BALOZI AISHA ATEMBELEA OFISI ZA TEMESA MAGOGONI, AFURAHISHWA NA UTOAJI HUDUMA KWENYE KIVUKO
Posted On: March 05, 2022
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Balozi Aisha Amour, leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua huduma zinazotolewa katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na kukagua, pia amesikiliza maoni ya wananchi kuhusu huduma zitolewazo katika kivuko hicho.
Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi kivukoni hapo, Balozi Aisha amesema kutokana na uwepo wa msongamano mkubwa wa abiria wanaosubiri kupata huduma, Serikali itatenga fedha za manunuzi ya kivuko kingine na kufanya idadi ya vivuko eneo hilo kuwa vinne
Amesema kuwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha huduma za vivuko pamoja na kupunguza msongamano wa abiria na magari kwenye eneo hilo.
“Tunatarajia baada ya kivuko hicho kuwasili, kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 500 Sawa na abiria 2,000 na magari 60 na tayari fedha zimeshatengwa kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2022/23”. Amesema Balozi Aisha.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala amesema serikali imefanya maboresho ya ukataji tiketi kwa kusimika mfumo mpya wa kielekroniki (N-CARD) wa kusimamia mapato katika eneo hilo.
“Mfumo huo unaondoa mfumo wa zamani wa kutumia tiketi za karatasi na tayari tumeona mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa abiria katika sehemu ya kukatia tiketi,” alisema Kilahala.
Ameongeza kuwa abiria ambao wanatumia kivuko hicho kwa nadra wamewekewa utaratibu wa kadi za muda watakazozitumia wakati wa kuvuka katika eneo hilo.
Mtendaji Mkuu Kilahala amesema kivuko cha MV.KAZI kimepelekwa kwenye matengenezo na kinatarajiwa kurejea baada ya miezi mitat