MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA
Posted On: July 03, 2020
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unashiriki Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maaarufu Sabasaba ambayo yameanza mnamo Tarehe 1Julai.
Banda la TEMESA katika maonesho hayo lipo ndani ya (Holi la KARUME) na maonesho hayo yanatarajiwa kufungwa ifikapo Julai 13, mwaka huu wa 2020.
Maonesho ya Sabasaba yanafanyika katika viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika barabara ya Kilwa na yanatoa fursa ya kutafuta masoko ya mazao na bidhaa za kilimo, viwanda na huduma nchini.
Kauli mbiu ya Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) kwa mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu inayolenga kutambua mchango wa Sekta ya Kilimo na Viwanda katika kuzalisha ajira na kujenga biashara endelevu".