WADAU WA TEMESA MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA KAZI ZA MATENGENEZO (MUM)
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania umeendelea kuendesha mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo (MUM) kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi kutoka taasisi za serikali kuhusu matumizi ya mfumo huo wa kidijitali. Mafunzo hayo, yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Adden Palace Hotel na kuwakutanisha pamoja Maafisa Usafirishaji kutoka taasisi mbalimbali za serikali Mkoani Mwanza, pamoja na wawakilishi wa karakana teule zilizosajiliwa na TEMESA.