BUNGE LAPITISHA BAJETI YA TRILIONI 2.28 KWA WIZARA YA UJENZI
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mei 06, 2025 limepitisha kwa kishindo Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ya Shilingi trilioni 2.28 baada ya mjadala wa kina uliohitimishwa na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega. Akizungumza wakati wa kuhitimisha mjadala huo, Waziri Ulega amesema bajeti ya Wizara hiyo imeongezeka kutoka trilioni 1.6 hadi trilioni 2.28, sawa na ongezeko la asilimia 28, hatua ambayo inalenga kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo katika Sekta ya Ujenzi.