MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AKAGUA VIVUKO VIPYA VITANO MWANZA
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko vipya vitano kati ya sita vinavyoendelea kujengwa na Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA). Vivuko hivyo vipya vinaendelea kujengwa na mkandarasi Songoro Marine katika yadi yake iliyoko Ilemela Mkoani Mwanza na tayari vimefikia wastani wa asilimia zaidi ya 92%. Vivuko hivyo vinatarajiwa kuanza kutolewa kwa ajili ya kutoa huduma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.