TEMESA YAENDELEA NA MAFUNZO YA MFUMO WA MUM KWA LENGO LA KUBORESHA NAMNA BORA YA UTOAJI WA HUDUMA ZAKE
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA umeendelea kutoa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo (MUM) kwa wadau wake katika mikoa mbali mbali nchini ukiwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma zake kwa wadau na kuipunguzia Serikali mzigo wa madeni. Mafunzo haya yamefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha yakiongozwa na Mhandisi Pongeza Semakuwa, ambaye pia ni Meneja wa Kikosi cha Umeme TEMESA na kuhudhuriwa na maafisa usafirishaji kutoka taasisi za serikali, wamiliki wa gereji teule zilizosajiliwa na TEMESA, pamoja na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali za kiserikali.