WATUMISHI TEMESA MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA KIDIGITALI WA MUM
Watumishi wa karakana ya TEMESA Mkoa wa Mwanza Leo wamepatiwa mafunzo maalumu kuhusu namna ya kutumia mfumo mpya wa kidigitali wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo MUM. Mafunzo hayo yamefanyika katika karakana ya TEMESA Mkoa wa Mwanza iliyoko eneo la Igogo na kuendeshwa na Mkufunzi wa Mfumo huo ambae pia ni Meneja wa kikosi cha Umeme, Mhandisi Pongeza Semakuwa na kuhudhuriwa na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Frank J Msyangi pamoja na watumishi wa TEMESA kutoka mkoa wa Mwanza. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mhandisi Semakuwa amesema mfumo huo utawezesha TEMESA kufuatilia kazi za matengenezo kwa wakati, kuweka kumbukumbu sahihi za majengo, na kutoa taarifa za kiutendaji zinazosaidia maamuzi sahihi.