TEMESA NA KONGAMANO LA WANAWAKE KANDA YA KATI

Mikoa ya Kanda ya Kati Dodoma, Singida na Iringa leo imefanya kongamano ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8, jijini Arusha. Kongamano hili lenye kaulimbiu “Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji kwa Wanawake na Wasichana 2025.” limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kujumuisha wadau mbalimbali wa serikali, asasi za kiraia, na jamii kwa ujumla, wakijadili jinsi ya kufikia malengo ya usawa na uwezeshaji wa wanawake na wasichana katika nyanja mbalimbali za maisha. Katika hafla hii, mada zilizojadiliwa ni pamoja na jinsi ya kuhamasisha jamii kutambua na kuthamini haki za wanawake, kuboresha usawa katika maeneo ya kazi, elimu, na afya, na kuhakikisha kuwa wasichana wanapata fursa za kipekee za kujikwamua kiuchumi