DKT MSONDE AKUTANA NA MENEJIMENTI YA WAKALA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, amekutana na kufanya kikao cha kazi na menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) katika ukumbi wa mikutano wa TEMESA makao makuu jijini Dodoma leo Februari 24, 2025. Kikao hiki kimefanyika kama sehemu ya majumuisho ya ziara yake katika karakana mbalimbali za wakala, ambapo Dkt. Msonde amehimiza utekelezaji bora wa majukumu ya taasisi na umuhimu wa mshikamano katika menejimenti ya wakala.