ULEGA AZINDUA AZAM SEA TAXI, AWATAKA WAVUVI KUTOTUPA NYAVU HOVYO BAHARINI.
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaojishughulisha na uvuvi maeneo ya Kigamboni kutunza mazingira na kutotupa nyavu katika njia inayopita vivuko ili viweze kutoa huduma ya kuvusha wananchi kwa ufanisi na ubora. Ulega ametoa agizo hilo leo Januari 23,2025 jijini Dar es Salaam wakati akikagua na kuzindua vivuko viwili vitakavyofanya safari za Magogoni - Kigamboni vinavyomilikiwa na Kampuni ya Azam ambavyo vitapunguza adha ya usafiri kwa wakazi Dar es Salaam hususan wananchi wa maeneo ya Kigamboni.