​‘’TUENDELEE KUIUNGA MKONO SERIKALI YETU KWASABABU NI SERIKALI SIKIVU NA INATATUA KERO ZA WANANCHI,’’ MTENDAJI MKUU TEMESA

Mtendaji Mkuu TEMESA Lazaro Kilahala na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko Mhandisi Sylvester Simfukwe pichani wakiagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho ya vivuko katika kituo cha Ilunda-Luchelele pamoja na Ijinga-Kahangala ambao unaendelea. Serikali inatarajia kupeleka kivuko kipya eneo la Ijinga-Kahangala na tayari TEMESA inaendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu ya kivuko hicho ili kitakapokamilika kiweze kuanza kazi mara moja.