​WAZIRI ULEGA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI WIZARA YA UJENZI.

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi katika Ofisi ndogo za Wakala ya Barabara (TANROADS), leo tarehe 11 Disemba, 2024 Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour, pamoja na Wakuu wa Taasisi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N. Kilahala, Wakala ya Barabara (TANROADS), Wakala wa Majengo (TBA), Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) na Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT).